Natanguliza shukrani zangu za dhati kwa mwanzilishi wa blog hii kaka GEOFREY MALWA, nampongeza sana kuona kuna umuhimu wa kizazi cha sasa kupewa masomo na makungwi mbalimbali ili kuweza kuokoa matatizo mengi yanayojitokeza katika mahusiano.
Kwa majina naitwa Kungwi Aisha a.k.a nyonga mdebwedo. Na mada yangu mezani siku ya leo ni kuhusu "NYETO" nawalenga hawa wanaume zetu wenye jukumu nyeti uwanjani.
Kwa wanaume wote wanaofanya mchezo huu watambue kuwa sio mchezo salama kwa afya ya dhakari zao. Na vinavyotuua ni vitu viwili vikubwa...
1. Mitandao ya kijamii
Tunaitumia vibaya mno. Walioitengeneza nahisi wanatusikitikia jinsi hii mitandao ilivyotuzidi nguvu. Kukodolea macho picha za utupu za wakinadada, video mbalimbali za wadada wanaofanya umalaya mtandaoni, na kubwa zaidi ni kuangalia video za ngono. Kama mwanaume unayafanya haya yaache mara moja, yatakupelekea upunguze hamu ya tendo na mwisho wa siku uingie kwenye kundi kubwa la wanaume wanaotafuta busta za asili kila kukicha.
Tena sasahivi mpaka vijana wanaupungufu, hili tatizo lilikuwa ni la wazee sasa jiulize vijana wameingiaje? Tumieni mitandao kuzalisha na burudani iwe ni sehemu ndogo tu. Kwa usalama wa afya zenu, nawaomba muachane na vitu hivyo, ni bora usome hadithi za kusisimua kwasababu huoni picha wala video, maandishi hayana madhara yeyote, picha na video za ngono ni hatari kwa afya ya dhakari.
2. Vyakula
Zingatia milo yako ya siku, iboreshe kwa kuweka kipaumbele vyakula vya asili. Utamu wa chakula ndio wengi tunaufuata lakini hatuwi makini chakula hicho kitamu kinakwenda kuongeza nini mwilini. Punguza kutumia mafuta mengi. "Unavyokula ndivyo ulivyo" huu msemo una ukweli kwa asilimia kubwa sana. Hakikisha kwa siku, vitunguu swaumu na tangawizi visikose kinywani mwako, iwe ni kwa kupitia chakula au vinywaji kama chai, au kwa kutafuna/kumeza.
MUHIMU:
-Kufanya mazoezi ya viungo
-Kupata muda wa kupumzika
-Usiwaze sana ngono.
Usiposhtuka mapema babu wewe, basi utashtuliwa na manyoya ya mkeo, maana ukiona manyoya ujue....malizia mwenyewe.
Comments
Post a Comment