Kuna kausemi kanasema kuwa “Ulimwengu umejaa watu wenye roho mbaya na wenye chuki hivyo huhitaji kuwa mmoja wao kwa kujichukia na kujidharau!” lakini kwa bahati mbaya kuna watu wengi ambao hujichukia, hujidharau na kujiona kama takataka, huwathamini watu wengine kuliko wanavyojithamini wao na mara nyingi hutamani maisha yao yangekua tofauti na kuwa kama ya wale ambao wanawaona wao kama wana furaha jina wamafenikiwa.
Nikweli kuna wakati kila mtu anajichukia, anachukia namna alivyo na kutamani mambo yangekua tofauti, ni jambo la kawaida lakini kama kila siku wewe unajichukia basi si kawaida. Kuna sababu nyingi zinaweza kukufanya ujichukie, labda unajiona mbaya, huna kazi nzuri, hauko katika mahusiano, unaumizwa kila mara na nyingine nyingi. Kama huna furaha na kwa namna flani unajichukia basi jua hakuna upendo utakaotosha kukufanya kuwa na furaha mpaka pale utakapojifunza kujipenda wewe mwenyewe.
(1) Kwanini Unajichukia/Mapungufu Yako; Hatua ya kwanza kabisa ya kujipenda ni kutambua ni kwanini unajichukia, kuna kitu ambacho unakiona hakiko sawa katika maisha yako ndiyo maana unajichukia, maisha yako yangekua sawa basi usingekua na chuki juu yako. Hembu anza kwa kukiangalia hicho kitu, watu wengi hujichukia kutokana na namna wanavyoonekana, labda hajajaliwa shape flani, ni mnene sana, au mwembamba sana, anakitambi, anajiona mrefu sana au mfupi sana.
Mwingine huchukia weupe wake na mwingine weusi wake, kuna ambao hujiona wana nywele mbaya, sura imekauka na vitu vingine vingi, lakini wengine si muonekano, wengine hujichukia sababu ya kabila lao, dini zao, kazi zao, hujiona wana kazi mbaya au hawana uwezo mzuri darasani. Tambua hicho kitu, hicho ndiyo hukunyima furaha na kukufanya ujione kama huna thamani, ni kitu ambacho hata watu wakikupenda na kukusifia bado unajiona huna thamani kwakua unajiona hujakamilika, kitambue.
(2) Jua Kuwa Unaweza Kubadilisha Mapungufu Yako; Kama binadamu unatakiwa kujua kuwa unaweza kubadilisha hicho unachokiona mapungufu, inawezekana si kukibadilisha moja kwa moja bali kwa kukipenda au kujifunza namna ya kuishi nacho. Hili ni muhimu, kuwa hicho unachokiona mapungufu kinaweza kuabdilika, kama ni kazi unaweza kuanza kwa kuipenda, kuangalia uzuri wake, kuiangalia kwa namna chanya.
Ukasema hii kazi si nzuri sana lakini kwa upende mwingine basi inakupa chakula, ukaangalia mtaani watu ambao hawana ajira kabisa ukaona wanavyoteseka. Kama ni maumbile yako, tusema hujalaaliwa kalio na unajichukia, ukamshukuru Mungu kwakua kuna ambao hawana miguu kabisa, kuna ambao hawawezi kunyanyuka wamelemaa, ukajiangalia kama kitu chanya kwamba namna ulivyo ndivyo ambavyo Mungu alitaka uwe na ni baraka kwako.
Ukajua kuwa mapungufu unayoyaona yako kwenye akili yako, si kila mtu anakuona hivyo unavyojiona kuna watu wengi wengi wanakuona umefanikiwa, wanaona una maisha mazuri na hata kutamani maisha yako. Kwa maana hiyo basi ukaacha kuwa mtu wa kulialia na kuangalia vitu vingine, ukaangalia baraka nyingine, ukaitoa akili yako kabisa kwenye vitu ambavyo hukuliza kila siku na kuipeleka kwenye vitu ambavyo hukupa nfuraha.
(3) Tambua Watu/Vitu Ambavyo Hukukumbusha Kujisikia Vibaya; Wazungu wanaita ‘Triggers’ vitu ambavyo vikitokea au watu ambao ukikutana nao wanakufanya ujisikie vibaya na kuzidi kujichukia. Wanaweza kuwa ni marafiki zako, mume/mke wako au wafanyakazi wenzako, kila ukionana nao wewe ni kujilinganisha nao, au hata kama hujilinganishi lakini kazi yao ni kuorodhesha mapungufu yako, utasikia mtu mwenyewe hivi, una hiki, huwezi hiki na vitu kama hivyo.
Unapokua karibu nao unajiona mdogo, unajiona huna thamani au hujafanikiwa hata wasipo sema chochote. Kama ni watu basi unatakiwa kujua kuwa pamoja na dharau zao, pamoja na wewe kuwaona kama wamefanikiwa nao kama wewe wana mapunfufu yao, wanalia kivyao na kwanamna flani hasa wale ambao kila siku nikukukosoa wanatamani maisha yako, wako chini na wanataka kukudhau ili uwe chini kama wao, usiwaruhusu na wachukulie kama wanadamu ambao huumia pia acha kujilianganisha nao.
Lakini inawezekana ni vitu au wewe mwenyewe, labda ukijiangalia kwenye kioo ukaona sura yako, ukivaa nguo unaona hupendezi, ukifanya kazi unajiona huwezi na vitu kama hivyo. Kumbuka wewe ni mwanadamu si lazima kuweza kila kitu na jinsi ulivyo inatosha, unapojiangalia kwenye kioo acha kuangalia mapungufu bali alngalia ulivyobarikiwa, hupendi makalio yako angalia macho yako yalivyo mazuri, hupendi miguu yako angalia nywele au kifua chako utajikuta huumii sana.
(4) Acha Kujaribu Kumdidhisha Kila Mtu; Unapokua katika hali hii, unapokua unajichukia utajikuta unataka watu wakupende, ili ujisikie vizuri utatamani watu waone mazuri yako, wakutamani, wakuweke karibu. Kwasababu hiyo wakati mwingine unaweza kujikuta unakua mtu wa “Ndiyo Mzee!” unajaribu kumridhisha kila mtu ili ufiti na kuwa kama yeye, ili uwe na marafiki ukidhani kuwa ukijiweka karibu na mtu flani labda ndiyo utakua na furaha hapana.
Acha kujaribu kuridhisha kila mtu, acha kuishi maisha ya watu, unatakiwa kujua kuwa kwanza huhitaji kupendwa na kila mtu na pili hutakuja kupendwa na kila mtu, acha kujipendekeza, badala ya kutumia muda mwingi kutaka kuwa kama flani, kutaka flani akupende basi tumia muda huo kujipenda wewe na kuishi maisha yako. Utajikuta baada ya muda kila mtu anakupenda, anafurahia kuwa na wewe na hakuna mtu anayeyaona mapungufu yako kwakua huna haja ya kujishusha ili kuwa na furaha.
(5) Acha Kufikiria Sana; Unapokua unajichukia mara nyingi kila kitu unakifikiria mara tatu tatu, kila kosa hulioni kama la kibinadamu bali lakwako unajiona huna akili na ni mtu ambaye hana thamani. Mfano umefeli mtihani, umeshindwa kufanya kazi falani unawaza mara nyingi nyingi, hujisamehi kutokana na makosa, uko kwenye diet umekula chakula cha mafuta, unatumuia kutwa nzima kuwaza kuhusu hicho chakula mpaka unachanganyikiwa. Acha kufikiria sana kama kosa limetokea limetokea, kama umefanya kitu kibaya chukulia poa, jifunze na endelea na maisha yako.
(6) Acha Kuficha Kitu Unachokichukia; Mara nyingi unapokua unajichukia, unachukia kitu flani katika maisha yako unajaribu kukificha ili wengine wasikione, unakionea aibu. Kwa mfano unataka kupungua una tumbo unakua unaficha na mikanda, huna kazi unadanganya, huna hela ya kula lakini unajitutumua kutoa michango ya harusi, kwakifupi unakua muoga muoga watu kujua ukidhani watakuona nusu mtu au huna akili hapana.
Sisemi utangaze mapungufu yako hapana, lakini usijisikie vibaya kuwa ulivyo, kwamfano kama hujajaliwa kalio acha kuona aibu kuvaa skin tight za kuboost kisa unaogopa watu, vaa na ukiona wanakusengenya waambie “Napenda nikivalia na jeans…” Mbona wao wanavaa mawigi, huna hela ya kula mtu anahitaji mchango muambie kabisa kwasasa siko vizuri na si kujitutumua. Usitangaze mapunfufu yako lakini usiyaonee aibu, yakubali na wengine watayakubali utajikuta unakua na furaha.
(7) Kila Mtu Ana Mapungufu Yake; Nadhani hiki ni kitu ambacho watu wengi wanaojichukia hawakijui au hawataki kuamini, kila mwanadmau ana kitu ambacho anakichukia katika maisha yake, ndiyo maana wanasema kuwa hakuna mtu aliyekamilika. Huyo unayemuona ana kitu flani unakipenda na kutamani kuwa kama yeye kuna ambacho hana na yeye naakitaka hicho tu kimoja, anasema ni bora ningenyimwa hiki nikapewa kile.
Hivyo acha kujiona mpweke, kujiona kama wewe ndiyo umebeba matatizo ya dunia na kujichukia, kuna wengi kama wewe na wengi wanaojichukia usiwaze sana! Usijisikie vibaya kwa kuwa namna falani au kukosa kitu flani, kumbuka kuwa kila mtu ana kitu alichokosa na kamwe huwezi kuwa na kila kitu, unapoanza kujisikia vibaya angalia vitu ambavyo wewe unavyo na wengine hawana, shukuru na jua kuwa ni kama mmebadilisha na wewe una hiki na wao wana kile.
(8) Samehe Na Jiruhusu Kukosea; Hakuna nguvu kubwa katika kuwa na furaha kama kujifunza kusamehe, kwanza kwa kujisamehe wewe mwenyewe na pili kwa kusamehe wengine, ulishajiangalia vibaya, kuna mtu alikusema vibaya, kuna mtu ambaye alikuumiza zamani, ulikosea kitu flani mpaka ukagombana na mtu au kukosa kitu flani, hembu jisamehe na msamehe mhusika, hata kama hajakuomba msamaha lakini fanya hivyo, jiondolee sumu ya chuki ndani ya moyo wako.
Kumbuka kuwa tunaumia zaidi kwa kuchukia wengine kuliko kufanyiwa mabaya. Lakini pia wewe ni binadamu jiruhusu kukosea, acha kujipima kama mkamilifu, acha kujiaangalia kama mtu ambaye hapaswi kukosea. Utakosea, jaribu tena na jisamehe. Hata wewe utajaribu kumshuha mtu mwingine, utafanya kitu kibaya, utamuumiza mtu mwingine acha kuishi na maumivu, kujihukumu bali tambua wewe ni binadamu na jisamehe maisha yaendelee.
(9) Acha Kusikiliza Ubongo Wako; Kama una tatizo hili kila siku ubongo wako utakua unakukumbusha mapungufu yako, kila siku utakua ukikumbuka kosa flani ambalo ulilifanya siku flani, utajaribu kukuambia uko hivi kwasababu falani, ungefanya hivi ingekua vile na mambo kama hayo. Kwakifupi utakua unakusuta na kukuambia mambo hasi kila siku, acha kuusikiliza, acha kuruhusu mawazo hasi kutambaa kichwani kwako, unaweza usiwe na nguvu au mwema kiasi hicho lakini usiruhusu ubongo wako kukufanya kama huna akili kabisa.
(10) Wewe Ni Binadamu Huwezi Kufanya Kama Mungu; Untakiwa kujua kuwa wewe ni binandamu, huwezi kufanya kila kitu, huhitaji kufanya kila kitu, huwezi kujua kila kitu na hakuna anayejua kila kitu, lakini pia huwezi kuwa na sifa zote, huwezi kuwa na muonekano mzuri ambao utampendeza kila mtu, jua wewe ni wakipekee, umeumbwa kwa namna yako hivyo huhitaji kufanya miujiza, huhitaji kufanya maajabu zaidi ya kuwa wewe, acha kujaribu kumfurahisha kila mtu.
Acha kujaribu kufanya kila kitu, acha kujaribu kufanikiwa katika kila kitu, nisawa kushindwa, nisawa kutokuweza baadhi ya mambo, hauko peke yako wengi tu hawawezi kitu unachotamani kukiweza na wengi tu wanatamani kuwa kama wewe na kufikia hata nusu ya mafanikio yako, lakini hawawezi si kwasababu ni wajinga si kwasababu niwavivu hapana ni kwakua tu ni wanadamu hivyo acha kutaka kuwa Mungu kuwezi kufanya kila kitu.
Comments
Post a Comment