UAMINIFU KATIKA MAHUSUANO

UAMINIFU KATIKA MAHUSUANO




Watoto wawili, Mvulana na msichana walikuwa wakicheza pamoja. Mvulana alikuwa na Goroli na Msichana alikua na Pipi. Mvulana akamwambia msichana kwamba wabadilishane golori kwa pipi, Msichana alikubali.

Msichana akachukua pipi zake zote na kumpa mvulana kama walivyo kubaliana, lakini Mvulana alimpa baadhi ya goroli na kubakiza moja ambayo ilikua ni nzuri kuliko zote.

Usiku ulipofika, msichana akaenda kulala kwa amani. Lakini Mvulana hakuweza kulala kwa amani kwakua alikua akiwaza huwenda msichana yule hakuwa mwaminifu kama yeye na hakumpa pipi zote.

Somo la hadithi: Kama hutokua muaminifu kwa asilimia 100 kwenye Mahusiano yako, usitegemee kua na amani na furaha na Uhusiano huo. Tulizana! Chukua hatua.

Comments