Ndoa Iheshimiwe Na Watu Wote

Ndoa Iheshimiwe Na Watu Wote



GBTW: Kufanikiwa kwa ndoa hakuhitaji kuwa na pesa nyingi kwenye akaunti, nyumba kubwa na ya maana, au gari la gharama. Unaweza ukawa navyo vyote hivyo na bado ukawa unaona ndoa yako ni kama jela ndogo.

Kufanikiwa kwa ndoa kunahitaji Uaminifu, Commetment, kutokuwa na ubinafsi, na Mwenyezi Mungu juu ya yote. Mwanaume apataye mke, amepata kitu chema, Wewe kama mwanaume ishi na mwanamke wako kwa akili, akili huendana na hekima na busara, na umpende mke wako kama bwana alivolipenda kanisa.

Kadhalika ninyi wake, watiini waume zenu, kujipamba na kujiremba kwenu kusiwe kwa nje tu yaani kusuka nywele, foundation, make up, kucha etc, bali kuwe utu wa moyoni usioonekana, katika mapambo yasiyoharibika yaani roho ya upole na utulivu, ilivyo ya thamani kuu mbele za Mungu.

Wewe kama mwanamke tambua kwamba, upendeleo hudanganya, na uzuri ni BATILI, bali mwanamke amchaye Bwana ndiye atakaesifiwa.

Anafuraha mtu yule apatae rafiki wa kweli, ila anafuraha zaidi mtu yule apatae rafiki ambae ni mke au mume wake. Mungu ameumba jambo jipya, kwamba mwanamke atamlinda mume wake.

Ndoa iheshimiwe na watu wote, na wenye ndoa wawe waaminifu kwa wenzi wao ; maana Mungu atawahukumu wazinzi na waasherati.

Comments