Mapenzi Na Hasira
TGIS: Wakati baba akiwa anasafisha gari yake mpya aliyonunua kwa gharama, mwanae mwenye miaka saba alichukua jiwe na kuanza kuandika katika upande wa lile gari.
Kwa hasira baba alichukua mkono wa yule mtoto na kuanza kumpiga kwa nguvu bila kugundua kuwa alikua akitumia spana kumpigia hivyo akamuumiza vibaya.
Hospitalini wakapata report kuwa mtoto ameumia vibaya kupelekea mifupa ya vidole vyote kuvunjika hivyo inatakiwa kuondoa vidole vyote.
Mtoto alipomuona baba yake kwa uchungu na maumivu makali akamuuliza "Baba ni lini vidole vyangu vitarudi tena?" Baba aliumia vibaya sana moyoni na hakika hakua na la kusema.
Alirudi nyumbani na kulipiga gari lake mara nyingi kwa hasira, akiwa amekaa upande wa lile gari akatazama ni nini mwanae alichokua akiandika. Kuja kuona mwanae aliandika "NAKUPENDA SANA BABA YANGU". Siku iliyofuata Baba alijinyonga baada ya kushindwa kuhimili hisia za alichokifanya kwa mwanae.
Nini akidi ya kisa hiki??
MAPENZI NA HASIRA.
Hivi vitu viwili havina mipaka, chagua upendo ili uweze kuishi vizuri hapa duniani na achana na hasira. Vitu vinatakiwa kutumiwa na watu wanatakiwa kupendwa.
Ila kwa bahati mbaya dunia ya sasahivi mambo yamebadilika sana vitu vinapendwa na watu wanatumiwa.
Angalia mawazo yako huja kuwa maneno, angalia maneno yako huja kuwa matendo, angalia matendo yako huja kuwa tabia, angalia tabia yako huja kuwa mazoea na angalia mazoea yako huja kuwa ndio mwisho wako.
Unajua uhusiano uliopo kati ya macho yako? Yanalia pamoja, yanafumba pamoja na panapo furaha hufurahi pamoja ingawa hayajawahi kuonana hata siku moja. Marafiki ni nguzo mojawapo ya maisha na upendo ndio msingi wa maisha. Let love lead.
Comments
Post a Comment