Haya Ni Ya Kweli?

Haya Ni Ya Kweli?



Haya ni ya kweli?

1. Sio wanaume wote wanaopenda michepuko

2. Sio wanawake wote wana mwanaume zaidi ya mmoja

3. Kuna wanawake hawana Boyfriend kabisa

4. Kuna wanaume hawana muda kabisa na wanawake.

5. Kuna wanawake bado ni bikira hata kati ya umri wa miaka 18-30. Bikira zipo.

6. Kuna baadhi ya wanaume hawajawahi kulala na mwanamke ingawa wana miaka 20-30

7. Kuna baadhi ya watu wapo kwenye mahusiano bila ya kukutana kimwili. Wana date lakini hakuna sex, mpaka watakapooana.

8. Wanaume wote hawapo sawa. Sio wote wanaofikiri mwanamke ni chombo cha starehe. Wapo wanaoheshimu wanawake.

9. Wanawake wote hawapo sawa na sio wote huvutiwa na pesa katika mahusiano, wanachotaka ni heshima, upendo na uaminifu.

10. Kuna watu karne hii bado ni waaminifu, hawawezi kusaliti na kukusababishia maumivu ya kihisia.

Watu hutofautiana sana tabia kutokana na malezi na misimamo binafsi.

Je haya ni ya KWELI au UONGO. Niambie.

Comments