SHERIA ZA FAMILIA BORA

1. Kula Chakula Pamoja
Familia ambayo inakula chukula pamoja hukaa pamoja. Kula chakula pamoja huwa inasaidia wanafamilia kuwa karibu sana na kushare mambo yao ya siku nzima kwa pamoja. Ila sasa wakati wa kula kuna baadhi ya sheria ambazo unatakiwa kuweka
- Kula chakula kwenye meza ya kulia chakula na sio kwenye makochi
- Hakikisha tv inakua imezimwa wakati wa kula
- Wekeni simu mbali wakati wa kula
- Waambie watoto wawe wanaandaa meza kuweka sahani vijiko na maji.
- Waambie watoto watulie na kula chakula badala ya kucheza, maana watoto wenyewe muda wa kula pia huwa wanaendelea kucheza kwa hali hii wakiendelea nayo wakikua itakua balaa.
- Waambie watoto wasiongee wakati wana chakula mdomoni.
- Tenga chakula mezani ambacho mnaweza kukimaliza, hii pia inamfundisha mtoto umuhimu wa chakula.
- Usiharakishe muda wa kula, kuleni taratibu maana huo ndio mda wenu wa kuongea na kubadlilishana mawazo wakati mnakula
2. Fata Sheria za Barabarani
Huwa ni bora kufika salama kuliko kubadilisha njia na kuereka hospitali. Haijalishi una haraka au la....

Comments