1. Sherehe ya Harusi ni ya siku moja tu, na
Ndoa ni ya maisha yote.
.
2. Mwanamume/Mwanamke aliyezoea
kuchepuka kabla ya Ndoa, ataendelea
kuchepuka hata baada ya Ndoa.
.
3.Upole na ukimya si kiashiria cha tabia
njema.
.
4. Ukikitaka ambacho hakijawahi milikiwa
na mtu yeyote, ni lazima ufanye jambo
ambalo halijawahi fanywa na mtu yeyote
.
5. Mungu akitaka kukubariki hukuletea mtu, na Shetani akitaka kukuangamiza hukuletea mtu.
.
6. Bora uishi mwenyewe kuliko kuoa ama
kuolewa na mtu asiye sahihi.
.
7. Aina tatu za wanaume wakuepukwa:
(a) Walevi
(b) Wazinzi
(c) Wagomvi.
.
Aina tano za wanawake wa kuepukwa;
(a) Walevi
(b) Wazinzi
(c) Wachawi
(d) Wagomvi
(e) wasio tii
.
8 .Kuolewa na Mchekeshaji hakutakufanya
uwe na Ndoa yenye furaha.
.
9. Maneno matatu yanayojenga amani
katika Ndoa:
(a) Nakupenda.
(b) Samahani.
(c) Asante.
.
10. Kupiga punyeto kwa mwanaume na
kujichua kwa mwanamke ni kuharibu mwili wako mwenyewe.
.
11. Kuoana kabla ya kuwa marafiki ni kama gari bila mafuta. Hamuwezi kufika popote.
.
12. Mafanikio ya Ndoa siku zote ni
pembetatu:
>Mungu mmoja
> Mume mmoja
> Mke mmoja.
.
13. Furaha ya kudumu maishani hutegemea na chaguo lako la mwenzi ktk Ndoa.
.
14. Usioe/kuolewa na pesa au mali. Oa/
Olewa na mtu. Pesa/Mali hufilisika lakini utu hudumu milele.
.
15. Uchumba uliovunjika ni bora zaidi kuliko Ndoa isiyo na amani wala furaha.
.
16. Usiweke kipaumbele chako kwa
muonekano mzuri wa mwanamke. Hakuna mwanamke mbaya, bali anahitaji
kupendezeshwa.
.
17. Mapenzi si upofu. Upofu ni kuoa ama
kuolewa na mwanamume/mwanamke kwa sababu tu anakidhi haja zako kingono.
.
18. Ukiwa rafiki mwema, utawavutia
marafiki wema. Vivyo hivyo kwa marafiki
wabaya (Bad company corrupt good
character)
.
19. Asili ya mikono inayojali ni moyo
unaojali.
.
20. Iepuke Ndoa mbaya kabla haijaanza...
21. Mungu ndiye kiongozi na usalama wa ndoa yako usiache kumtumikia wakati wote.

Comments
Post a Comment