MPE AMANI - UTAYAONA MANUFAA YAKE.

Ushawahi kujiuliza kwanini mwanamke analia kirahisi anapoumizwa? Ni kwa sababu mwanamke hapendi matatizo. Pale alipo mwanamke, hua panakua na mpangilio mzuri ikiwemo na amani.
Muulize mtu yoyoye aliyefanikiwa, aidha atakwambia ni kwa sababu ya mama yake kumpa support au mke wake.
Mwanamke aliumbwa kuleta amani na mpangilio katika maisha. Hivyo kama sehemu hakuna amani na mpangilio mzuri mwanamke hawi comfortable hata kidogo.
Anaweza akaingia kwenye nyumba ambayo ni chafu na haina mpangilio akaisafisha na kuiweka katika order nzuri. Anaweza akamuona mwanaume wake mchafu, asie na mpangilio wowote wa maisha akajitahidi kuyaweka maisha yake kwenye order nzuri ingawa atakutana na vikwazo kutoka kwa mwanaume huyo ikiwemo kutosikiliza ushauri wake.
Mwanamke anafanya kazi yake vizuri mahali ambapo kuna mazingira ya amani na mpangilio mzuri.
Kutokana na hayo, hata kwenye MAHUSIANO, mwanamke anahitaji amani na hujitahidi kwa kila hali kuwe na amani. Ukiwa kama mwanaume, ni jukumu lako kutengeneza mazingira ya amani kwa ajili ya mwanamke wako. Hautakuja kuona ile potentiality ya mwanamke wako katika mazingira ambayo hayana amani.
Anapokuwa hana amani na wewe, mwanamke wako hujisikia hawezi kitu, ile nguvu yake ya ndani haiwezi kuonekana, ule uwezo wa usaidizi humpotea kabisa. Hautafurahia uwepo wa mwanamke katika maisha yako endapo patakua na mazingira yasiyo na amani kama vile vita vya Mosul na Aleppo huko Syria.
Kama ukitaka kumfaidi mwanamke wako, mpe amani na uhakika kwamba yeye ndio pekee na wala hashindani na pizza bandits pamoja na slay queens!
Mpe care na ile attention anayoihitaji, kuwa karibu yake pale anapokuhitaji msikilize huku ukimuangalia machoni..kuwa aina ya mwanaume wake ambae anao uhakika hata wa kuwaeleza watu wake wa karibu.
Mwanamke anapokua na amani, uhakika na kujiamini kwamba yupo sehemu sahihi, ile nguvu na uwezo wake huja automatically. Atakuombea mara kwa mara wakati ukihangaika kujitafutia kipato. Usitegemee mwanamke akuombee ufanikiwe wakati mafanikio yako ni mwiba kwake.
Unapomjali vizuri mwanamke wako alie bora, atakupa support ambayo hauwezi ku-imagine. Mungu husikia kilio cha wanawake. Mungu hujibu maombi ya wanawake. Huu ni ufahamu mdogo tu kwako my black brother!
My wisdom "When a woman is well treated, she will intercede for you in ways you can't imagine, God hears the prayer of woman. Don't push a woman to the point she starts praying dangerous."

Comments