*MPASUKO WA MOYO 💔🙆🏼*

Mpendwa ,kama umeamshwa salama tamka neno kwajili ya kumtukuza Mungu, maana wapo waliolala jana kama wewe na leo hawakuamka, jiulize kwanini wewe? tafakari upendo wa Mungu kwako .
*Mpendwa leo tuangalie moyo kwa kiasi , maandiko yanasema katika moyo ndiko ziliko chemichemi za uzima , Mpendwa hebu jitafakari ndani ya moyo wako umetunza nini?, yawezekana mwonekano wako wa nje hausadifu uhalisia wa wewe kwakuwa kuna vitu vimebebwa katka moyo wako na vimekwenda kuathiri chembechembe za uhai wa moyo wako, jitafakari wewe mwenyewe Moyo wako unafuraha au uchungu? Una amani au faraka? Jitafakari 🙇🏻*
Mpendwa yamkini kuna mambo hayajakaa vizuri katika maisha yako hii ni kwasababu moyo wako umetunza mambo ambayo si rafiki kwa ustawi wa moyo na matunda yake, yawezekana wazazi,ndugu jamaa au marafiki wameumiza moyo wako kwa maneno yao ya fedheha au matendo yao ya kikatili na kuumiza, na hayo yote moyo umeyatunza na mara uyakumbukapo tu moyo wako umekuwa ukisononeka na kushindwa kuruhusu utendaji kazi wa viungo vingine mwilini mwako na hivyo kukufanya wewe uonekane mpweke na dhaifu kama vile mtu aliyeachwa yatima jangwani 😭🙆🏼.
*"Linda moyo wako kuliko yote uyalindayo; Maana ndiko zitokako chemchemi za uzima*"
MITHALI 4:23 👆🏻
Mpendwa ili uwe salama mruhusu Roho Mtakatifu ajaye kwa upya moyoni mwako na wewe uwe tayari kusahau kumbukumbu zote mbaya na kutoa mizigo yote uliyokuwa umehifadhi katika moyo wako ili uwe huru ooooh hallelujah 😃💪🏼
*Mpendwa linda sana moyo wako, kwani mtu yoyote akitaka kuharibu maisha yako anacheza na moyo wako tu, ndio maana yakupasa uwe makini sana, usiruhusu tu kila mtu auchezee moyo wako, kabla hujaamua kuweka kitu au mtu ndani ya moyo wako tafakari kwa kina kama shauri hilo halitaacha vidonda ndani ya moyo wako* 💔
Mungu atusaidie sana tusijifanye tunamjua sana Mungu kiasi cha kuitoa mioyo yetu kwa kila mtu na hatimaye hufanywa dampo la kuweka kila takataka ambazo zikioza huleta harufu mbaya na kudhoofisha maisha yetu na mbaya zaidi dhamiri hufa na ndipo utu wetu hupotea , Mungu atupe nguvu za kustahimili haya yote.
* MOYO WAKO SIO DAMPO, KATAA KUHIFADHI UJINGA ILI UWE NA AMANI💉😂*

Comments