ILI NDOA YAKO IWEZE KUDUMU , BASI TAMBUA ' UPENDO ( Affection ) NI KITU MUHIMU KULIKO KUJAMIIANA ( SEX ).
Kwenye Mahusiano / Ndoa yoyote huwa yanatawaliwa na vitu viwili (I) UPENDO (Affection) (II) Kujamiiana (SEX).
Unapotaja hivi vitu viwili , Tambua : Kitu cha kwanza mwanamke anachohitaji umfanyie sana ni upendo , Mwanamke haitaji kujamiani kama anavyohitaji upendo na hawezi kujamiiana kwa amani kama hakuna UPENDO.
Upendo) sio kujamiana , wanaume wengi wanaamini kuwa wanapomaliza kujamiana mwanamke huwa ana furaha , Siyo lazima iwe kweli kwa sababu mara nyingi na wanawake wengi huwa na hasira pale waume zao wakisha fika kilele (their husband climaxes) kwa sababu wengi wao huwa wanakuwa hawajaridhika yawezekana kwa kutofika kilele au kutomaliza hamu zao.
Wanaume wengi huwa wanadhani kumfikisha mwanamke kilele ndiyo kukidhi Shauku yake, Jawabu ni " HAPANA " katika hali ya utimilifu/ukamilifu wa mwanamke anaweza kufika mshindo/kilele zaidi ya mara tatu hadi saba au zaidi ya hapo kwa tendo moja tu la mwanaume.
Bahati mbaya wengi wao wamepoteza uwezo huo kutokana na matatizo ya kihistoria , Hadi wengine kufikia hatua ya kuigiza wanafika kilele ilimradi tu kumridhisha mwanaume na kujiepusha na aibu ya kuonekana hawana hisia , Inapofika hapo " Hakuna namna yoyote ya kumfariji mwanamke zaidi ya UPENDO "
" Ndiyo maana tunasema Mwanamke anahitaji UPENDO ( Affection ) zaidi kuliko kujamiana "Na usipofanya hivyo kuna uwezekano mkubwa akatafuta Chaguo (option) nyingine ya kujitoa matamanio yeye mwenyewe au mtu mwingine , Hapa mahusiano hayatakuwa na uwezekano tena wa kudumu.
UPENDO NI NINI ?
UPENDO - inakubidi ufanye kitu maalum kwa mtu ambacho kitaleta matokeo na athari kwenye akili ya mtu.
UPENDO - mwanamke anahitaji kuambiwa kila siku na mumewe kuwa nakupenda na hii ni kila siku hata mara kumi kwani anahitaji hicho kama upendo wako kwake.
UPENDO - Ni kumpelekea maua mkeo bila hata sababu.
UPENDO - kushikana mikono mbele za watu na kutembea sehemu za mikusanyiko bila kuhofia chochote.
UPENDO - Ni kumwambia mkeo njoo ukae karibu yangu hata wakati Ukiendesha gar au una majukumu mengine muhimu bila kujali atakuvuruga.
UPENDO Ni kumpeleka mkeo kula chakula cha mchana au jioni kwenye mazingira tofauti ambayo hakuyazowea bila hata sababu.
UPENDO - Ni kumsaidia mkeo majukumu ya nyumbani bila kujali nani anakutazama - usione haya kumwambia nifundishe ..kupika ,kuosha vyombo, kumenya matunda ,kulea mtoto n.k.
UPENDO - Ni kumfungulia mkeo mlango wa Gari na kumfunga au kumfungua Mkanda kisha na busu kidogo.
UPENDO - Siyo kitu cha gharama ni kitendo cha kuwaza tu kitu kizuri cha kumfanyia mkeo ambacho kwa mtu mwingine hawezi kukipata kirahisi au kila wakati
UPENDO - Huanzia asubuhi, kucheza kitandani, kumbusu mkeo na kumuita majina mazuri hata kumwambia maneno mazuri na kujulisha kilichokufanya usiwaoe wengine ukamuoa yeye.
UPENDO - Nii kumbusu mkeo kabla hajaenda kazini au kabla ya wewe kuondoka kwenda kazini.
(upendo) ni kumpigia mkeo kila baada ya dakika kumi na kumwambia nimekupigia ili nkwambie tu nakupenda alafu kata simu hautaji kuongea saaaana inachukua sekunde tatu tu.
Kama bado unajidanganya mwanamke akitendewa haya anakuwa kiburi , MKE MWEMA UTAENDELEA KUMSIKIA KWA BONNY MWAITEGE.
Comments
Post a Comment