Moja ya vitu vigumu sana kwa wanawake kuviacha baada ya kuolewa ni Sponsor hasa kama alikua anahudumia vizuri na mwanaume aliyempata sasa ni wale wa maisha ya kawaida kwamba hawezi kumpa hata robo ya vitu alivyokua anapewa na Sponsor. Mwanamke huyu anakua ashazoea aina flani ya maisha ambayo ni ngumu sana kuyaacha kwani hujiona kama mfungwa flani hasa kama kakubali kuolewa si kwa upendo bali kwakua anaona umri unaenda.
Lakini mwingine ni kwa upendo ila akiwaza mali na vitu alivyokua akipewa basi anachanganyikiwa. Lakini mwingine iko hivi labda kaachana Sponsor kwamba hawakutani na kufanya mapenzi tena lakini bado wanawasiliana hivyo akiwa na shida anamuambia Sponsor na anamsaidia bila kumtaka kingono. Wanawake wengi hapa hudanganyika na kudhani labda ma-sponsor wana roho nzuri wanaheshimu kua kaolewa bila kujua wanawekeza na ipo siku watakuja kukutana na kutaka uwekezaji wao.
Sasa wanawake wengi walikua na ma-sponsor ingawa uwezo wanatofautiana lakini wapo sasa wajanja wakishaolewa huagana na kufuta mawasiliano yote lakini wale wanaojiona wajanja sana basi hawa hudhani kua wanaweza kula kotekote. Sasa inawezekana mwanaume ulikua unajua au ulishahisi kua ana Sponsor au hujui lakini kuna dalili ambazo ukiziona kwa mkeo hembu kabla hujapaniki ongea naye vizuri kujua kuna nini kinaendelea.
(1) Ana Matumizi Ambayo Hayaeleweki, Makubwa Kuliko Kipato Chake; Inawezekana anafanya kazi au hafanyi kazi lakini matumizi yake ni makubwa sana ukilinganisha na kipato chake. Lakini ishu si ukubwa wa matumizi tu, bali aina ya matumizi yake ndiyo yanakushangaza. Anawekeza pesa zake katika kununua mawigi ya ghali kuliko mshahara wake, nguo za gharama kuliko mshahara wake na matumizi mengine ambayo hata si ya msingi. Akikuomba hela ukimuambia huna anayafanya mwenyewe.
Iko hivi wanawake wanapenda matumizi lakini hawapendi kutoa hela zao katika mambo ya kijinga watataka kutumia pesa za mtu mwingine. Mwanamke hata kununua chakula wakati mwingine ni shida, sasa kama unaona mkeo ananunua tu vitu ambavyo kwanza havieleweki lakini pili ukipigia mahesabu mshahara wake hautoshi basi hiyo ni dalili ya kwanza. Kua makini chunguza ujue kwani hata ukiuliza basi atakudanganya.
(2) Kaka/Ndugu Zake Wana Msaidia Sana Wakati Unajua Hali Zao Ni Mbaya; Umegundua matumizi yake mwanzoni alikua haongei lakini baada ya kuhoji utasikia Mama kanipa Shilingi flani, alikuomba hela ya kitu flani kwakua hana lakini ghafla anaseama Kaka yake kampa, sijui ndugu zake wamemsaidia. Inawezekana kweli wana hela lakini unawaza hivi kweli wampe hela kwaajili ya kutoka out na marafiki zake au kwaajili ya kununua Iphone mpya.
Lakini unaona kabisa hayo matumizi ambayo anayataja ndugu zake kwa hali zao unaona kama hawana uwezo nayo. Haiingii akilini na kama ukihoji sana hataki uongee nao kuhusu hilo swala na kama ikitokea ukauliza atakasirika na kununa akisema unataka kumgombanisha na ndugu zake. Wanawake wengi hutumia njia hii kwani wanajua kuwa ni ngumu kwa mwanaume kuwapigia ndugu wa mke kuwauliza kama wamempa Dada yao pesa.
(3) Kila Kitu Kipya Ni Mkopo Kazini Au VICCOBA Ambayo Huijui; Mara ghafla kachukua mkopo tena bila kukubaliana na wewe kanunua Gari. Lakini umevumilia unawaza hili Gari atalihudumiaje anakuambia mshahara bila kukumbuka aliuchukulia mkopo, haiishii hapo anajisahau matumizi yake ni yale yale pamoja na mkopo na ukimuuliza mara anakuambia ninacheza mchezo, anakuambia nina kikundi cha VICCOBA.
Katika vitu vyote hivyo unashangaa ni mikopo gani hii anachukua kwaajili ya kufanya vitu vya anasa na si vitu vya maendeleo? Lakini ukifuatilia zaidi unaona kuwa kama ana mikopo kila sehemu hayo marejesho yanatoka wapi wakati matumizi yake ni makubwa namna hii. Ndugu yangu sisemi anachepuka lakini kama mikopo yake ni kwaajili ya kununulia vitu vya anasa basi ni wakati wa kuchunguza vizuri kabla hujajuta msije mkalipa wote.
(4) M-Pesa Yake Iko Bize Kama Vile Ni Mfanyabiashara; Aanaweza kuwa makini kuzifuta meseji lakini kila mara ukiangalia unakuta kwenye simu yake, iwe ni M-Pesa, Tigo Pesa au nyingine kuna hela tu. Hujui zinatoka wapi kwani hata kama anafanya biashara halipwi kwa simu au hata kama anafanya kazi mshahara hauingii kwa simu. Lakini ukiwa makini ukaingia kwenye meseji za Mpesa utakuta kuna mtu mmoja anatuma tuma sana.
Lakini anaweza asiwe mtu, labda akajifanya mjanja sasa ukakuta kuna namba moja ya wakala ambayo inamtumia pesa kila siku au namba ambayo imeseviwa jina la kike inatuma pesa mara kwa mara. Kama ukigundua ukauliza atakuambia kuwa kuna mtu nilikua namdai. Ukiona hivyo kuwa na mashaka kidogo na chunguza kwani kwakua hana uhuru wa kuonana na Sponsor wake basi hutumia simu kuombe hela.
(4) Ghafla Anapata Hela Ya Kutatua Matatizo Yenu Kutoka Kwa Rafiki Ambaye Humjui; Gari yake imegongwa na alikua hana hela ghafla unaona kazipata ukimuuliza katoa wapi maelezo yake hayaeleweki, mara kuna mtu tulisoma naye, sijui ofisini kumetokea hiki. Lakini kuna tatizo nyumbani na alikua hana hela ghafla zimetokea na hakuna maelezo ya kueleweka. Kwa kifupi matukio yanapotokea yeye anakua na hela za ghafla na hazieleweki zimetoka wapi.
Iko hivi akili za binadamu katika matatizo ni kutafuta suluhu ya haraka, wakati wazo la kwanza kwa mwanaume anapopata tatizo ni kukopa kwa mwanamke ni kuomba na mtu rahisi kutoa hela kwa mwanamke ni mwanaume wake wa zamani mwenye hela ambaye bado wanawasiliana, ambaye bado ana matumaini atakuja kumpata na kumtumia kingono. Si kila mwanamke anafanya hivyo lakini kama ni kitu cha kujirudiarudia kila siku ni wakati sasa uwe makini na mkeo.
(5) Safari Ambazo Hazieleweki; Kwa mwanamke ambaye anahudumiwa tu lakini hatumiwi kingono basi anaweza asiwe na safari hizi, lakini kwa yule ambaye anatumika kingono basi kuna wakati inabidi akalipe deni la watu. Hivyo kwakua mwanaume huyu naye atakua ameoa na mara nyingi hatataka kumtumia mchana kwakua yuko bize na mbaya zaidi atataka kumtumia vizuri basi atataka kuonana naye kwa usiku mzima.
Sasa kama mkeo ana dalili hizo hapo juu, matumizi yake hayaeleweki na kila mara anakua na safari za kijinga jinga, yaani mara anasingizia za kikazi wakati ukichunguza kazini hamna kitu. Au ni za kikazi lakini hakuna barua hata ya kuonyesha kweli anaenda hiyo safari, lakini misiba ya rafiki zake ambao hata huwafahamu, mara nyingi si ndugu kwani ndugu unawafahamu utataka kwenda au utapiga simu.
Misiba inakua ni ya marafiki wa chuo na mara kwa mara atakua akisema anaenda na rafiki yake mmoja. Kwamba huyo rafiki yake atapiga simu ili usikie na ujue wameenda wote usiwe na wasiwasi basi jua kuwa anaenda kulipa hela za watu. Hemu chunguza anapotaka kwenda hizi safari za misiba au kwenda kwenye Kitchen Party hasa za weekend ambazo hazina hata kadi (hawasemi harusi utataka kwenda) basi kua makini na chunguza.
Nimalize kwa kusema acha kukurupuka hizi ni dallili tu inaweza kuwa kweli au si kweli. Hivyo kabla ya kukasirika na kuanza kuropoka hembu anza kuchunguza kimya kimya, chunguza kuhusu matumizi yake, kuhusu safari, kuhusu pesa za ghafla, kuhusu VICCOBA, kuhusu hilo Gari alilonunua na nani analifanyia services. Usikurupuke tu utajua na ukijua muambie tu aache huo ujinga kwani ushajua, lakini nawewe jitahidi kuhudumia vizuri!
Nimekuambia hivi si lengo umuache mke wako hapana, lengo ni kuiokoa ndoa yako kwani baadhi ya wanawake wakishaingia katika mtego wa fedha hujisahau sana, madhara yake si kwako tu bali watoto. Usisubiri mpaka umfumanie na wala usitake kumfumania ila kama umeona dalili na unahisi kitu ongea naye na muambie kuna dalili umeziona awe makini kwani siku ukimfumania unamuacha na huo mchepuko wake ndiyo utakata kamba mazima!
Comments
Post a Comment